
Na William Mpanju- KAGERA
Wagombea udiwani viti maalum walioshinda kura za maoni wilaya ya Biharamulo mkoa Kagera, wametakiwa kutojiamini kuwa wameshinda kwa ngazi ya udiwani baadala yake watambue kuwa mchakato wa kuwateua unaendelea kwa taratibu za Chama Cha mapinduzi CCM kupitia jumuiya ya wanawake UWT.
Hayo yamesemwa na msimamizi wa uchaguzi wa umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi UWT Bi Chiristina James wakati akitangaza matokeo ya waligombea udiwani viti maalum katika tarafa ya Lusahunga na Nyarubungo.
Amesema matokeo ya kura ya maoni udiwani Viti maalumu Jimbo la Biharamulo magharibi imekuwa kama ifuatavyo
Tarafa ya Lusahunga
Wagombea walikuwa 08, jumla ya kura zilizopigwa ni 1351, kura zilizoharibika ni 47, kura halali ni 1304.
1. Hawa Idrisa Rubatona kura 42
2. Angelina Kasabo kura 64
3. Avelina Salabaga kura 67
4. Joyce mayala kura 70
5. Sauda seleman kura 97
6. Zuhura Mmango kura 592
7. Frolentina Charles Matiba kura 671 na
8. Zyuni Hussein kura 980.
Tarafa ya Nyarubungo
Wagombea walikuwa 10, idadi ya wapiga kura walikuwa 1238, kura zilizoharibika ni 39 kura halali ni 1199.
1. Beatrice oganga Ayuko kura 939.
2. Maryam Mwesa Bundala kura 681
3. Afisa Abubakari Gariatano kura 922
4. Shella chalse kamando kura 124
5. Edina Tibalebwamunda Melchades kura 284
6. Ashura khamis Mussa kura 461
7. Amelia aloyce Nyakake kura 749
8. Mansura Abdulkarim Omary kura 102
9. Asia Nuru RUBATONA kura 816
10. Hamida Issa seleman kura 195.
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo SACP ADVERA BULIMBA amewataka wanawake ambao kura hazikitosha kuendelea kuwa wazalendo kwani hizo ni kura za maoni na mchakato unaendelea na kuwasihi kuendelea kuwa wamoja na kulinda amani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.