William Mpanju- Biharamulo, KAGERA
Wagonjwa wa kifua kikuu wametakiwa kujiepusha na unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara ambao unapelekea kuchangia kuongeza kasi vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu ambapo madhara yake kifo.
Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma wilaya ya Biharamulo Dkt. Tumpale Akimu amesema hayo wakati akizungumza na Radio Kwizera juu hali ya mapambano dhidi ya kifuu kikuu na madhara yake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya ukoma duniani ambayo hufanyika Machi 24 kila mwaka.
Amesema Kifua kikuu kinaenezwa kwa njia ya hewa hasa kwenye mikusanyiko ya watu ikiwemo magulio, migodoni na kwamba kutokana na elimu inayoendelea kutolewa ikiwemo kutumia dawa kwa usahihi na matibabu yake ni bure
Baadhi ya wagonjwa wa kifua kikuu waliopona ugonjwa huo wamesema changamoto inayochangia wagonjwa wa kifua kikuu kutopona ugonjwa huo ni pamoja na kushindwa kuzingatia masharti hasa kuendelea kutimia pombe na sigara na kukatisha dozi ya dawa.
