
Idadi ya vifo vya watu waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa Nyandolwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani humo imeongezeka, na kufikia saba baada ya kuokolewa kwa miili ya watu wengine wawili wakati wa zoezi la uokoaji likiendelea.
Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Mboni Mhita wakati akielezea mwenendo wa zoezi la uokoaji katika mgodi huo, ambapo mpaka sasa watu 10 wametolewa kati ya 25 waliofukiwa na kifusi, kati yao 7 wamefariki na watatu wako hai.
Aidha Bi. Mboni amesema kuwa zoezi la uokoaji linaendelea ili kuhakikisha wanawapata watu 15 ambao bado wamenaswa chini ya aridhi na watu wote watakabidhiwa kwa ndugu zao.
Leo ni siku ya 11 tangu watu 25 ambao ni mafundi katika mgodi wa kikundi cha wachapa Kazi, eneo la Nyandolwa, halmashauri ya Shinyanga
wafukiwe na kifusi wakati wa kutekeleza majukumu yao.