
Serikali kupitia wizara ya afya, imeendelea na zoezi la ugawawaji wa vyandarua katika mikoa mbalimbali nchini ambapo May 27, 2025 wananchi mkoani Kigoma wamenufaika na kampeni hiyo ya kupata vyandarua bure ili kuendelea kupambana na ugonjwa wa malaria
Akizindua zoezi hilo mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye, katika zahati ya Lusimbi manispaa ya Kigoma Ujiji amesema kwa mwaka 2024 wagonjwa waliothibitika kuwa na maambukizi ya Malaria kwa mkoa wa Kigoma ni 3,9080 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ni 264.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa hali hiyo sio nzuri, watoto wanapokufa wengi zaidi kwa ugonjwa wa malaria kuliko watu wazima na kuwataka wataalam kuendelea kusisitiza utekeleza wa afua zote, afua za kinga lakini pia afua za tiba na kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Nao Wananchi wameishukuru serikali kwa msaada huo kwani umewasaidia kupunguza gharama za kwenda kununua vyandarua madukani, kwa wale wasiojiweza na itasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na malaria