Samwel Masunzu- Kibondo, KIGOMA
Wananchi kijiji cha Kitahana, kata ya Kitahana wilayani Kibondo mkoani Kigoma wamechangia kiasi cha shilingi milioni 3 kwaajili ya kutengeneza madawati kwaajili ya shule za msingi zilizopo kweye kata hiyo
Kabla ya zoezi la kukabidhi madawati hayo 42 kwa shule tatu za msingi Kasebuzi Muyaga na Kahama Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kitahana Bi. Doto Omary amesema upungufu kwa shule zote ni madawati 297.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kitahana Bw. Eriabi Kabuga amesema kupitia kamati zake walipita kwenye shule hizo na kubaini changamoto ya uhaba wa madawati na kuidhinisha kiasi cha milioni 3 kutengeneza madawati, fedha ambayo ni nguvu za wananchi.
Katibu wa Mbunge kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Bi. Dorice Sekela amesema Ofisi ya Mbunge itatoa madawati 71 yenye thamani ya sh. Milioni 5
