
Wanawake katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani Geita Mkoani Geita wametakiwa kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbogwe Bi.Grace Abel wakati akizungumza na wanawake Katika mji wa katoro ikiwa ni moja ya hamasa yake inayo endelea ndani ya mkoa wa geita kuhamasisha wanawake na uongozi.
Bi.Abel amesema kumekuwa na dhana potofu inayojengeka ya kwamba wanawake ni viumbe dhaifu lakini dhana hiyo ni potofu kwani wapo baadhi ya wanawake ambao wanafanya vizuri kazi katika nafasi mbalimbali walizo nazo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wanawake ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa katoro Bi.Fatuma Nasoro amesema mwanamke ni msingi katika familia hivyo haina budi kila mwanamke kuhakikisha anakuwa kiyoo ndani ya jamii kwa kusimamia misingi bora ya maadili kwa watoto wao.