Samwel Masunzu- Kibondo KIGOMA
Baadhi ya waoteshaji wa miti ya kutunza mazingira wilayani Kibondo mkoani Kigoma wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya upandaji wa miti itakayosaidia katika kutunza mazingira na kupunguza hewa ukaa.
Hayo yameelezwa na Bw. Eliakimu Bitabo pamoja na Bi. Seili Eliakimu wakati wakizungumza na Radio Kwizera kwenye bonde la kijiji cha Kumwambu kata ya Kumwambu.
Wamesema upandaji wa miti husaidia kuzuia ongezeko la hewa ukaa na kuongeza kinga dhidi ya mafuriko na mmomonyoko wa udongo hasa maeneo yenye mwinuko.

Hata hivyo mpango wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma ni kupanda miti milioni 1 na laki 5 kila mwaka kutoka wakala wa huduma za misitu TFS ambao wamekuwa wakiwagawia wananchi miti ya kupanda kwenye maeneo yao.
