
Na Samwel Samsoni- SHINYANGA
Uchaguzi wa madiwani wa viti maalumu wilaya ya Kahama yenye majimbo matatu ya uchaguzi na Tarafa sita, (Kahama Mjini, Ushetu na Msalala) imeanza jana Julai 20, 2025 majira ya asubuhi katika jimbo la Kahama Mjini, na kutamatika alfajiri ya leo Julai 21, 2025.
Katika uchaguzi huo uliokuwa na wajumbe 3807 umempitisha kwa kishindo Mwenyekiti wa umoja wa Wanawake wa CCM wilaya ya Kahama Thelesphora Saria kwa kura 1093, akifuatiwa na Vaileth Bulili aliyepata kura 1041.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi Ernestina Richard amesema jumla ya watia nia 23 wamechaguliwa kwenye nafasi hiyo .
Amewataja wengine katika tarafa ya Kahama Mjini jimbo la Kahama Mjini kuwa ni Eritha Makaga amepata kura 954, Rehema Joshua 948, Mary Boniface 314.
Tarafa ya Isagehe ni Scolastika Kahanya amepata kura 840, Mpaji Mlekwa 839, Winifrida Peter 462.
Katika jimbo la Msalala, Tarafa ya Msalala, Mariam Ngeleja ameongoza kwa kupata kura 933, Nyagwema Warioba 650, Hamisa Kalinga 567, Grace Masanja 547.
Tarafa ya Isagehe Msalala, Pili Izengo kura 499, Mwashi Mgeja 501 na Martha Shadrack 478.
Jimbo la Ushetu, Tarafa ya Dakama ni Felista Kabasa 767, Yulitha Msafiri 765, Betha Leonard kura 733, Maria Maziku 421 na Eva Pius 514.
Tarafa ya Mweri ni Asha Marco 1053, Ester Matone 1042 na Hellen Musiba 612.
Akizungumza kwa njia ya simu leo Julai 21, 2025, katibu wa UWT wilaya ya Kahama Happiness Mpena amewataka walioshinda kuwa watulivu, kuvunja makundi na kuungana pamoja ili wajijenge kuelekea kampeni za uchaguzi mkuu.
Awali watia nia 90 walijitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa katika nafasi hiyo, baada ya vikao vya ndani watia nia 66 waliokidhi vigezo waliteuliwa ambapo siku ya jana julai 20,2025 wamepigiwa kura na washindi waliopatika a katika majimbo yote matatu ni 23 tu.