Msanii Travis Scott ameweka wazi kwamba watoto wake hawaruhusiwi kutumia teknolojia ya AI au hata kuangalia TV.
Hii ni kutokana na kuwepo na hatari ya akili zao kushindwa kukua kikamilifu ikiwa watategemea AI. Lazima wajifunze kwa njia ya kawaida, kwa mwili na akili, ili baadaye wajue jinsi ya kutumia AI kwa ufanisi.
Amesema ikiwa AI inafanya kila kitu kwao, je, watajua nini ni sahihi na nini si sahihi?. Watoto wangu hawaruhusiwi kutumia AI wala TV”
Travis Scott ana watoto wawili, Stormi wa miaka 7 na Aire Webster wa miaka 3, watoto wa pamoja na Kylie Jenner.
Kwenye mahojiano na Rolling Stone, Travis Scott pia alionyesha jinsi baba anavyopata mtazamo mpya wa maisha kupitia uzazi.
Travis Scott hajaridhika na teknolojia kwa watoto. Tayari alizungumza kuhusu hili mwaka 2018 akisema, “Watoto leo wako kwenye iPads na teknolojia nyingi, hawaendi kucheza nje. Ndiyo maana, kwa Stormi hakuna TV. TV ipo nje.”
Kwa Travis Scott, msingi ni kuhakikisha watoto wanakua wakiwa na akili za kutatua matatizo na ubunifu kabla ya kutumia teknolojia ya kisasa.