
Serikali wilayani Biharamulo mkoani Kagera imewaonya watumishi wa halmashauri hiyo wanaoshindwa kuwajibika katika nafasi zao na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Biharamulo SACP Advera Bulimba amesema hayo wakati akiongea na watumishi na wakuu wa idara wa halmashauri hiyo juu ya uwajibikaji katika nafasi walizopangiwa.
Amesema baadhi ya wakuu wa idara hasa wakuu wa shule za msingi na sekondari wanashindwa kusimamia nafasi walizopewa kwa kujihusisha na vitendo visivyoendana na maadili yao, hivyo kusababisha wananchi kuichukia serikali.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Bw. Innocent Mukandala amesema atafuatilia wakuu wa idara wasiowajibika ipasavyo katika nafasi zao ili hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa dhidi yao.