Samwel Masunzu- Kibondo, KIGOMA
Semina ya neno la Mungu inatolewa ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya Pasaka ya kumbukizi ya kifo na ufufuko wa Bwana Yesu Kristo ambayo ni sikukuu ya Ukombozi.
Akifundisha katika semina hiyo, mchungaji Geofrey Daudi katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) Agape Kibondo mjini amesema kila mmoja anapaswa kuwa na chanzo cha mapato ambacho kitamwezesha kupata urahisi wa sadaka na uchumi imara wa kuendesha familia yake.


Katika semina hiyo ambayo imeanza Machi 25 itakayotamatika Machi 29, 2026, Mchungaji Daudi amesema aliyeanzisha huduma ya utoaji ni Mungu mwenyewe kwa kutoa bustani ya Eden, kumtoa mwanawe wa pekee (Yesu Kristo) pamoja na kutoa nchi kwaajili ya wanadamu katika uumbaji wake wa mbingu na nchi na kwamba ili upate cha kutoa lazima uwe na mahali panapokuezesha kupata cha kutoa

Awali mchungaji mwenyeji wa kanisa hilo, Makamu Askofu wa jimbo la Kigoma Kaskazini Mch. Robert Luhumbi amesisitiza washiriki wa semina hiyo kuzingatia mafundisho yanayotolewa na kuyafanyia kazi
Baadhi ya washiriki na waumini wa kanisa hilo Bi. Jackline Venance na Bw. Wisdom Zabila wakiongea na redio kwizera wamesema matarajio yao katika semina hiyo ni kupata mabadiriko ya kimwili na kiroho hasa katika utumishi ndani na nje ya kanisa.

