Naomi Milton- Kigoma
Watu wawili wanasadikiwa kupoteza maisha huku wengine wanne wakiokolewa kufuatia ajali ya mtumbwi uliozama katika mto Luiche usiku wa kuamkia Machi 11 mwaka huu mkoani Kigoma.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa Opareshen wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kigoma Ngawipa Litaunga amesema juhudi za kuwatafuta waliopotea zinaendelea ingawa hadi sasa miili ya wanaodhaniwa kufariki bado haijapatikana.
Kufuatia ajali hiyo baadhi ya wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali kuharakisha kukamilisha ujenzi wa daraja lililokuwa karibu na mto huo jambo ambalo litasaidia kurahisisha usafiri na kupunguza ajali zinazojitokeza
Kwa upande wake diwani wa kata ya kagera katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Gregory Kabelezo amesema Daraja hilo limekamilika kinachosubiriwa ni uwekaji wa kifusi upande wa pili wa barabara ili kuruhusu matumizi rasmi.
Bofya Link neno -> KWIZERA TV au picha hapo chini kutazama

