Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ametoa Pole kwa familia zilizo poteza ndugu zao wakati na baada ya baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.
Waziri Dkt Nchemba ametoa pole hizo wakati akizungumza katika Mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, leo Novemba 25-2025.
Dkt. Mwigulu amesema matukio ya umwagaji damu ya yaliyofanyika siku hizo kuna waliofariki bila kushiriki vurugu hizo na hivyo ni kipindi cha watanzania kukemea viashiria vya kuirudisha nchi katika yaliyopita.
Aidha, amesema watu wanaochochea vurugu nchini wa nania ya kuiingiza Tanzania katika machafuko na wao kupata nafasi ya kupora rasilimali yake na kwamba Tanzania Italindwa kikamilifu na rasilimali zake.