
Katika mwendelezo wa kutoa elimu na msaada wa kisheria timu ya kampeni ya Mama Samia Legal Aid’ imezifikia shule mbili za msingi za Kata ya Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera.
Kampeni hiyo imezifikia shule za msingi Rulenge na Munjebwe na kutoa elimu ya namna ya kujilinda na kuchukua hatua panapotokea ukatili.
Akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Rulenge Wakili Baraka Samula amesema ni vyema wanafunzi kutambua haki zao na namna ya kujilinda na ukatili hasa kwa wanafunzi
Kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ya Mama Samia inaendelea wilayani Ngara kwa muda wa siku 9 ikilenga kuzifikia kata 10 na vijiji 30.