
Wananchi katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wanaoishi maeneo ambayo nyumba zao hujaa maji pindi mvua zinaponyesha wametakiwa kuchukua tahadhari ya kwenda maeneo salama ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
Rai hiyo imetolewa na kutoka kitengo cha mazingira kinachojihusisha na mambo ya maafa katika kanisa la KKT dayosisi ya kaskazini magharibi pamoja na shirika la TCRS Bw. Danson Kateme wakati akizungumza na Radio kwizera na kueleza kuwa ili kuwa salama ni muhimu wananchi wakachukua hatua ya usalama wao wakati wa mvua zinaponyesha.
Aidha baadhi ya wananchi ambao wanaathirika na maji katika nyumba zao wakati wa mvua zinaponyesha Bw;Anacret Byamungu, Bi;Ameriani Waagira pamoja na Bw;Rameck Vedasto waeiomba serikali kuwapatia makazi ya muda lakini pia kuiomba serikali kutengeneza miundo mbinu bora itakayopisha maji vizuri na kuepusha mafuriko katika nyumba zao.