
Wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS wilaya ya Chato mkoani Geita amesema ameweka mkakati wa kukuza uchumi wa kaboni katika wilaya hiyo kwa kuwafundisha vijana mbinu Bora za upandaji wa miti katika mazingira.
Mkuu wa hifadhi ya shamba la miti Silayo wilayani humo mhifadhi mwandamizi wa misitu Juma Mwita ameeleza hayo wakati akiongea na radio Kwizera juu ya namna ambavyo idara hiyo imejipanga kukuza uchumi unaotokana na misitu (kaboni)
Amesema zaidi ya vijana elfu ishirini wamekwisha jiandikisha kwa ajili ya kupatiwa mafunzo na kwamba kwa wale watakaokua na mashamba watapewa miche bure ili wakalisaidie taifa kuhamasisha uchumi utokanao na mazao ya misitu.
Mkuu wa wilaya ya Chato Louis Bura amesema mkakati huo ni mzuri na una manufaa katika uhifadhi wa mazingira na kuwataka vijana wa wilaya hiyo kuhakikisha wanachangamkia fursa za upandaji wa miti na kwamba biashara ya mazao ya misitu ina soko la uhakika.