
MWANZA
Na, Fred Seleli
Wawakilishi wa Tanzania mkoani Mwanza katika Kongamano la Kiswahili nchini Uganda kuanzia kesho April 14 hadi 16, 2025, wametakiwa kuwa wazalendo na kuutangaza uhodari wa Lugha hii adhimu.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa Peter Kasele ametoa wito huo jana wakati akiwakabidhi Bendera ya Tanzania ofini kwake.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wameahidi kuiwakilisha vema Tanzania katika kuchangia mijadala na shughuli zitakazoweka msingi wa mustakabali wa Kiswahili katika kizazi kijacho.
Kongamano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Kiswahili 2025 – 2050 inayolenga kukuza na kuimarisha matumizi ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano, elimu, biashara na utangamano katika ukanda wa Afrika Mashariki na Bara zima.