
Na, Jerome Robert
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman anatarajiwa kuminyana na Rais wa sasa wa Zanzibar Hussein Mwinyi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba baada ya yeye kujaza fomu za kugombea kiti cha Rais wa kisiwa hicho.
Othman ambaye alipokea stakabadhi hizo mapema leo, amewataka wanachama kumpa ridhaa akiamini uwezo mkubwa alionao kuongoza Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2025.
Othman amesema kuwa hatua hii inatokana na kuwepo haja ya kuleta mabadiko ya kiuongozi Zanzibar na kuamini kwamba Chama cha ACT Wazalendo ndio mbadala wa kuiondoa CCM madarakani.
Kwa upande wake Naibu katibu wa Chama hicho Zanzibar Omar Ali Shehe amesema hamasa kubwa ya uchukuaji wa fomu kugombea nafasi tofauti za chama imeongezeka tangu kuanza kwa zoezi hilo.
CHANZO: Mwananchi