
Baadhi ya wananchi katika vijiji vya Bugarama Mumiramira na Rwinyana wilayani Ngara mkoani Kagera wamejitokeza kupata elimu na msaada wa kisheria kutoka kwa timu ya Kampeni ya ‘Mama Samia Legal Aid’
Hayo yamejiri baada ya uzinduzi wa Kampeni hiyo uliofanyika April 15, 2025 na kuzinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi katika kijiji cha Bugarama.
Akizindua Kampeni hiyo Kanali Kahabi amesema ni vyema kuitumia fursa hiyo ili kupata uelewa wa masuala ya kisheria pamoja na kutatuliwa changamoto zao.
Katika kampeni hiyo wataalamu wa msaada wa kisheria wa Mama Samia wametoa elimu juu ya namna wanavyoweza kutatua migogoro ya ardhi, mirathi, ukatili wa kijinsia na kupata uelewa juu ya masuala ya kisheria.