
Jamii wilayani Ngara mkoani Kagera imetakiwa kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia miongoni mwa familia ili kujenga ustawi wao.
Hayo yameelezwa na Inspekta Khadija Mfinanga wa Dawati la Jinsia wilayani humo akiwa mjumbe wa timu ya Kampeni ya ‘Mama Samia Legal Aid’ katika kata ya Muganza.
Inspekta Mfinanga amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia umekuwa chanzo cha mifarakano na hata familia kutengana na watoto kubaki wakiteseka pasipo malezo sahihi.
Timu ya Msaada wa Kisheria ya ‘Mama Samia Legal Aid’ inaendelea na Kampeni ya kutoa elimu na msaada wa kisheria kwenye vijiji 30 ndani ya kata 10 za wilaya ya Ngara.