
Katika kuhakikisha jamii inaendelea kunufaika na kuwa na usawa katika umiliki wa mali, wananchi wametakiwa kutoa haki kwa mwanamke kumilii ardhi.
Akizungumza wakati wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, Afisa Ardhi wilaya ya Ngara Bw Cosmas Rubambura amesema mwanamke ana haki ya kumiliki ardhi kama ilivyo kwa mwanaume.
Bw Rubambura amesema iwapo haki hii itatolewa na kutekelezwa na wanajamii itasaidia kuondoa migogoro ya ardhi.
Aidha timu ya Msaada wa Kisheria ya ‘Mama Samia Legal Aid’ inaendelea na Kampeni ya kutoa elimu na msaada wa kisheria kwenye vijiji 30 ndani ya kata 10 za wilaya ya Ngara.