
Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imesema imezuia njama kubwa ya kumpindua kiongozi wa utawala wa kijeshi, Kapteni Ibrahim Traoré, ambapo inadai kuwa wapanga njama hao walikuwa wakifanya kazi kutoka nchi jirani ya Ivory Coast.
Waziri wa Usalama, Mahamadou Sana, amesema kuwa jaribio hilo la mapinduzi liliongozwa na wanajeshi wa sasa na wa zamani waliokuwa wakishirikiana na viongozi wa makundi ya kigaidi.
Aidha Waziri wa Usalama Bw Sana amesema kuwa mpango wao ulikuwa kushambulia Ikulu ya rais wiki iliyopita.
Lengo kuu, alisema, lilikuwa “kusababisha vurugu kubwa na kuiweka nchi chini ya usimamizi wa shirika la kimataifa.” Alitoa kauli hiyo kupitia televisheni ya taifa Jumatatu.