
Juhudi za kuwafikia wananchi wengi zaidi zimeendelea ili kutatua changamoto za kisheria kwa kutoa elimu na msaada wa kisheria.
Hatua hii imekuja baada ya Timu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kuongeza siku tano zaidi kwa mkoa wa Kagera.
Wilayani Ngara hatua hii imepokelewa vyema ambapo katika vijiji vya kata ya Bukiriro wananchi wamesema kampeni hiyo itasaidia kuzijua sheria.
Bw. Idd Kazoya wa kijiji cha Bukiriro na Bi. Monica Miburo wa kijiji cha Nyabihanga wamesema elimu hii itawasaidia kupunguza migogoro hasa ya ardhi na mirathi ambayo imekuwa changamoto katika maeneo yao.
Aidha timu ya Msaada wa Kisheria ya ‘Mama Samia Legal Aid’ inaendelea na Kampeni ya kutoa elimu na msaada wa kisheria kwenye vijiji 45 ndani ya kata 15 za wilaya ya Ngara.