
Na William Mpanju- Biharamulo
Mkuu wa wilaya Biharamulo mkoa Kagera SACP Advera Bulimba amewataka walimu kutumia taaluma yao kufundisha maadali kwa wanafunzi ili kuzalisha viongozi bora.
Amesema hayo wakati akifungua mkutano wa walimu mkoa Kagera uliofanyika katika Wilaya ya Biharamulo, ukiwa na lengo la kufanya uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa Kagera.
Amesema kuwa walimu wananafasi kubwa katika utoaji wa maadili kwa wanafunzi katika makuzi yao.