
Aliyekuwa naibu wa rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, baadae leo anatarajiwa kuzindua chama kipya ambacho anasema kitatumika kumng’oa Ruto madarakani katika uchaguzi ujao.
Kulingana na vyanzo vya karibu na Rigathi, chama atakachokizindua kitafahamika kama Democracy Citizens Party (DCP), ambacho kilisajiliwa mwezi Februari mwaka huu.
Jumanne ya wiki hii, Gachagua na washirika wake waliripotiwa kukutana faragha kupanga na kuamua uongozi wa chama hicho na namna ya kuzuia uuingiliaji wa serikali.
Gachagua na washirika wake wanamtuhumu rais William Ruto kwa uongozi mbaya wakiahidi kumshinda katika uchaguzi mkuu wa 2027.
Miongoni mwa wanasiasa wanaohusishwa na chama cha Rigathi ni pamoja na Kalonzo Musyoka, aliyewahi pia kuwa makamu wa rais, Martha Karua, Eugene Wamalwa na Fred Matiang’i, waliohudumu katika serikali ya Uhuru Kenyatta.