
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Saidi Mtanda amesema atazidi kushirikiana na wafanya biashara wadogo wadogo pamoja na vijana ili kuwatengenezea mazingira rafiki kwa ajili ya kundi hilo kujiajili kutoka na changamoto ya ajila kwa sasa
Ameyasema hayo jana wakati akifanya mkutano na viongozi wa maafisa usafirishaji wa makundi mbalimbali (Madereva Bodaboda, Bajaji na Guta) wa mkoa wa Mwanza na kuwaalika rasmi kushiriki kwenye ziara ya Mhe. Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuanzia Juni 19 – 21 jijini Mwanza.
Aidha amesema kwa sasa serikali haiwezi kuajili watu wote hivo wafanyabiashara hao wadogo hawatakiwi kubezwa hasa pale wanapofanya biashara hizo kwa ajili ya kujipatia kipato chao ndio maana serikali imezidi kuboresha mazingira ili vijana hawa wajiajili
Sambamba na hayo mkuu wa mkoa wa Mwanza said mtanda amezungumza juu umuhimu wa kuzingatia kutunza amani hasa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu 2025