Wananchi katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wanaoishi maeneo ambayo nyumba zao hujaa maji wakati wa mvua wametakiwa kuchukua tahadhari na kujiweka katika maeneo salama ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Wito huo umetolewa na wadau wa mazingira na maafa wakisisitiza kuwa hatua za kujikinga mapema ni muhimu, hususan kipindi cha mvua nyingi, ili kupunguza hatari ya mafuriko na uharibifu wa mali.
Baadhi ya wananchi walioathirika mara kwa mara wamesema wanahitaji msaada wa makazi ya muda na miundombinu bora itakayopitisha maji kwa ufanisi, ikiwemo uboreshaji wa mitaro na maeneo ya kupitisha maji ili kupunguza mafuriko kwenye makazi.
