
Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Geita mkoa wa Geita limesema litaendelea kuchukua hatua kwa madereva wa magari ya kubeba abiria wanaobainika kutumia vileo
Kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Geita Phabiano Daniel amesema hayo wakati wa zoezi la ukaguzi wa magari ya abiria kituo cha mabasi mjini Geita
Daniel amesema mkakati huo ni wa kudhibiti ajali za barabarani zitokanazo na uzembe wa madereva na matumizi ya vileo
Aidha Kaimu afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini LATRA mkoa wa Geita Mukiya Juma amesema mamlaka imekuwa ikiwachukulia hatua madereva ambao wanazaidisha nauli pasio kufuata taratibu za kisheria