
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wameiomba serikali kupunguza gharama ya ununuzi wa nishati safi ikiwemo gesi ili kuwezesha wananchi kutumia nishati hiyo na kuepuka uhalibifu wa mazingira wa kutumia mkaa na kuni.
Wakazi hao wamesema hayo wakati wakiongea na Radio Kwizera juu madhara ya kutumia mkaa na kuni jambo ambalo linachangia kutokea kwa madhara makubwa ya kiafya na uhalibifu mkubwa wa mazingira.
Miongoni mwa wakazi hao Bw Alfred Joas , Mathayo Makenzi na Grald Alfonce wamesema wanalazimika kutumia mkaa na kuni kwa sababu upatikanaji wa nishati safi vijijini ni changamoto pia gharama ya kununua gesi ni kubwa kutokana na uchumi wa wananchi ni mdogo,hali ambayo inachangia uhalibifu wa mazingira.
Hivi karibuni makamu wa Rais wa Tanzania Dr Philip Mpango amesema serikali inaendelea kuzungumza na makampuni yanayohusika na usambazaji wa gesi kuhakikisha wanapunguza gharama na hali ya nishati ya umeme inaendelea kuimalika ili kuwawezesha wananchi kutumia nishati hiyo ili kuepuka uhalibifu wa mazingira.