
Idara ya uhamiaji mkoa wa Geita imewakamata na kuwarudisha nchini mwao raia wa kigeni 126 kutoka nchi jirani ya Burundi baada ya kuingia nchini Tanzania kinyume na utaratibu
Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Geita James Mwanjotile amesema wahamiaji hao wamekamatwa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Geita katika oparesheni iliyofanywa na idara ya uhamiaji.
Aidha Mwanjotile amesema kuwa hadi Juni 30, 2025 idara ya uhamiaji imewakamata na kuwarejesha makwao raia wa kigeni 593 idadi kubwa ni kutoka Taifa la Burundi na wengine kutoka mataifa mengine ya Afrika Mashariki.
Hata hivyo Mwanjotile amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Idara hiyo pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kukabiliana na uingiaji holela wa raia wa kigeni
Kwa upande wao baadhi ya raia hao wa Burundi Ndaijimana Helodi na Bizimana Gerlad waliokamatwa kwa kwa kuingia nchini kinyume na utaratibu wamesema walingia nchini Tanzania katika harakati za utafututaji wa maisha