
Shirika linalojishughulisha na ustawi wa wanyama hususani wanyama kazi kama punda la ASPA, limeitaka jamiii kuepuka kuwabebesha wanyama hao mizigo mizito kuzidi uwezo wao
Albert Mbwambo kutoka shirika hilo amesema hayo baada ya mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Geita juu ya kuripoti na kuibua matatizo ya wanyama katika jamii
Mbwambo amesema wanyama wanaobeba mizigo, wanabeba mizigo inayozdi uwezo wao na hii ni kutokana na kutokuwa na uelewa katika jamii kuhusu haki za wanyama hao
Hata hivyo Mbwambo ameitaka jamii kuendelea kuelemishana juu ya haki za wanyama na kila mmoja kuwa balozi wa kuripoti matukio ya wanyama kubebeshwa mizigo mizito