
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewasili katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga kwa ajili ya Ufunguzi wa Kampeni na kueneza sera za chama hicho.
Nchimbi amesema endapo chama hicho kikiaminiwa wataanzisha mashamba darasa 60, skim nne za umwagiliaji, soko la mazao, vituo vya afya vinne, shule za msingi 6, shule za sekondari 4, mikopo kwa vijana bilioni 2000, Ajira 7000 za walimu, na ajira 5000 kwa kada ya Afya, pamoja na kurasimisha biashara zisizo rasmi.
Ameyasema hayo wakati akisalimia wananchi katika kata ya Kagongwa Manispaa ya Kahama akitokea Manispaa ya Shinyanga