
Mgombea mwenza wa Urais kupitia chama cha mapinduzi Balozi Dkt Emanuel Nchimbi amesema kuwa chama hicho kimejipanga kuimarisha afya za wananchi endapo kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano.
Ameyasema hayo leo wilayani Ngara mkoani Kagera wakati wa mkutano wa kampeni za chama hicho na kusema ndani ya siku mia moja za mwanzo chama hicho kitahakikisha kinatoa bima ya afya kwa watanzania wote
Balozi Dkt Nchimbi amesema kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakipitia changamoto hasa katika swala la matibabu kwa kushindwa kumudu gharama.
Aidha Dkt Nchimbi amesema kuwa katika siku mia moja za kwanza watumishi elfu tano wa kada ya afya wataajiriwa ili kupunguza uhaba wa watumishi wa kada hiyo uliopo kwa sasa.