
Wanachama wa tawi la klabu ya Simba la Nyankumbu manispaa ya Geita mkoani Geita wamesherehekea uzinduzi wa tawi hilo kwa kutoa vitu mbalimbali ikiwemo sukari, biskuti, juisi na mafuta ya kupikia kwa watoto wenye mahitaji maalumu wa kituo cha Mbugani mjini Geita
Mwenyekiti wa tawi la Simba Uwanja- Nyankumbu bw.Yuda John Amesema wameamua kufanya hivyo ikiwa ni utaratibu wa klabu hiyo hasa katika kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa 2025/26
Makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba mkoa wa Geita bi. Husna Said amesema vilabu vingine pamoja na wanasiasa wanapaswa kuiga mfano huo kwa kuwakukumbuka watoto wenye mahitaji
Kwa niaba ya uongozi wa shule ya Mbugani, mwalimu mkuu wa shule hiyo bw. Bernad Elias amewashukuru wanachama hao kwa kuonyesha moyo wa kusherehekea na watoto waliopo katika shule hiyo
Shuguli nyingine ambazo zimefayika ni kufanya usafi katika shule hiyo na kuwanunulia kifurushi cha Azam watoto hao ili waweze kuangalia Simba Day kupitia runinga ikiwa ni ombi ambalo wameliwasilisha kwa wanachama hao wa Simba