
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Geita imewataka wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutenda haki wakati wa mchakato wa uchaguzi
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita James Ruge amesema hayo wakati wa mafunzo kwa maafisa hao kutoka halmashauri za Geita DC na manispaa ya Geita , mafunzo ambayo yamefanyika uwanja wa ofisi za TAKUKURU Geita
Ruge amesema endapo kila mmoja atatekeleza wajibu wake, zoezi la uchaguzi litakuwa lenye haki na huru
Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Geita Said Lipunjaje amesema kila mmoja anapaswa kuepuka makosa ya kisheria katika kuelekea uchaguzi hasa katika makosa ya rushwa
Amesema sheria inawatambua wasimamizi hao katika kufanikisha zoezi muhimu la uchaguzi utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu 2025, hivyo wanapaswa kuepuka kuonyesha upendeleo kwa wagombea na vyama vya siasa.
Nao baadhi ya washiriki wamesema watatekeleza maelekezo hayo ili kujiepusha na kuchukuliwa sheria kwa kushindwa kusimamia viapo vyao
Hata hivyo TAKUKURU mkoa wa Geita imesema itaaendelea kutoa elimu kwa makundi mengine ya wadau wa siasa, asasi mbalimbali na dini ili kujenga uelewa wa wajibu na haki kwa kila mmoja kabla ya siku ya uchauzi