
Zaidi ya shilingi billion 4 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ujenzi wa mifereji eneo la Katubuka ili kupunguza athari kwa wakazi wa maeneo hayo ambao wamekukuwa wakikumbana na adha kubwa kipindi cha masika.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro alipokutana na kuzungumza na wakazi wa maeneo hayo ambapo amewataka kuwa watulivu huku akiwasihi kutosikiliza maneno ya upotoshaji kutoka kwa baadhi ya watu kuhusu utekelezaji wa mradi huo.
Nyumba zinazoonekana pichani ni makazi ya watu ambao kwa Sasa wana matumaini ya kurejea katika makazi yao huku wengine wakisema viwanja vyao vilivyozama wanategemea kuvijenga