
Benki ya NMB wilayani Kibondo mkoani Kigoma imeahidi kuendelea na ushirikiano na tawi la Simba Kitahana wilayani humo ili kutatua changamoto zinazokabili tawi hilo pamoja na matawi mengine
Katika uzinduzi wa tawi la Kitahana la klabu ya Simba, mwakilishi wa meneja wa NMB Kibondo Bi. Ester Kambarage amesema ushirikiano huo unaendea sambamba na upatikanaji wa kadi za uanachama
Kambarage amesema benki hiyo imeingia mkataba katika kuandaa kadi za uanachama kwa vilabu hasa Simba na Yanga ili kurahisha huduma zikiwemo za kushiriki katika kushuhudia michezo mbalimbali kwa kupata tiketi za uwajani kwa haraka zaidi
Hayo yametokana na risala ya tawi hilo ambayo imesomwa na katibu wa tawi la simba Kitahana bw. Joram Elioza Bidya Katika uzinduiz huo
Mwenyekiti wa tawi la Simba Kitahana bw. Japhet Magwala amesema ushirikiano huo utaendeleza tawi hilo na kurahisha kupatikana kwa huduma za klub kwa wakati
Mmoja wa mashabiki wa klabu ya Yanga Kitahana bw. Reuben Chubwa amesema baada ya kupokea mwaliko kutoka uongozi wa tawi la Simba, amejifunza mengi ambayo wanatamani waweze kuyafanya katika kilele cha siku ya mwananchi
Amesema yapo mengi ambayo wamejifunza ikiwemo ushirikiano
Wanachama , mashabiki na viongozi wa klabunya Simba tawi la Kitahana Kibondo pia wameshiriki shughuli mbalimbali kama vile kufanya usafi katika zahanati ya Kitahana na kuchangia damu