
Mwenge wa uhuru umepokelewa leo wilayani Ngara mkoani Kagera katika uwanja wa mpira wa Miguu shule ya lukole ukitokea Wilayani Karagwe kwa ajili ya kukimbizwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo leo utakimbizwa katika halmashauri ya wilaya ya Ngara.
Akipokea Mwenge huo mkuu wa Wilaya ya Ngara kanal Mathias Julius Kahabi amesema mwenge huo utatembelea miradi 7 kwenye halmashauri ya wilaya ya Ngara .
Kanal Kahabi amesema miradi itakayo kaguliwa na kuzinduliwa na mwenge wa uhuru ni miradi yenye thamani ya shilling Billion 2.7 kwa halmashauri ya wilaya ya ngara ameyasema hayo leo hii katika uwanja wa mpira wa lukole High school.
Kwa upande wake mkimbiza mwenge Kitaifa Ismail Ali Ussi amempongeza mkuu wa wilaya ya Ngara kwa maadalizi mazuri ya kupokea mwenge nakuongeza kuwa mazingira kiujmla yako vizuri na watu wamejitokeza kwa wingi.