Maelezo ya Kipindi
Nje ya Dimba ni kipindi cha michezo kinachowapa wapenzi wa michezo wenye umri wa miaka 14 na zaidi uchambuzi wa kina wa michezo ya ndani na ya kimataifa kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi.


Muda wa Kipindi
Kipindi hiki hurushwa hewani Jumatatu hadi jumamosi, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 05:00 asubuhi.
Mfumo wa Kipindi
Kipindi cha Nje ya Dimba kina sehemu kuu zifuatazo:
- Nje ya Dimba 1 (09:00 – 09:40 Asubuhi)
- Uchambuzi wa michezo Kitaifa,
- Magazeti Kurasa za mwisho
- Mjadala
- HABARI KWA UFUPI: (10:00 – 10:05 Asubuhi)
- Nje ya Dimba 2 (10:10– 10:55 Asubuhi)
- Uchambuzi wa michezo Kimataifa,
- Magazeti Kurasa za mwisho
- Mjadala
Upekee wa Kipindi
Nje ya Dimba inachunguza kwa undani uchambuzi, mbinu, historia na hivyo kuhimiza ushiriki wa hadhira kupitia SMS, simu na majibu ya mitandao ya kijamii.
Nafasi ya Wadhamini (Matangazo na Ushirikiano)
Taasisi za elimu, mashirika ya michezo yanaweza kuongeza kupenya kwao sokoni kwa kutangaza kwenye Nje ya Dimba.

