Vijana wilayani Karagwe Mkoani Kagera wametakiwa kutobagua kazi za kufanya badala yake wanawaweza kujita katika sekta ya kilimo ili kujipatia kipato na kuepuka hali ya utegemezi katika jamii.
Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga Bw. Projest Kajuna wakati akizungumza na radio Kwizera ambapo amesema kutokana na changamoto ya ajira vijana wengi wamekimbilia sekta ya bodaboda.
Kajuna jambo hilo linatakiwa kutazamwa kwa umakini kwa kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakikosa abiria na kupelekea kukaa vijiweni bila kujishughulisha na kazi za kuwaingizia kipato.
Baadhi ya vijana mjini Kayanga akiwemo Samweli Makoe na Elias Nestory wamesema serikali inatakiwa kuhimiza umuhimu wa kilimo kwa vijana kwa kutoa elimu sambamba na pembejeo.
