Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Access showcase, Imemtangaza rasmi msanii wa mziki wa Hiphop Frida Amani(@Fridaamaniofficial) kuiwakilisha Tanzania katika tamasha hilo litakalofanyika jijini Tshwane Nchini afrika kusini Novemba 1.
Tamasha hili ambalo kwa mwaka 2024 lilifanyika nchini Rwanda, hukutanisha wasanii, wadau wa muziki na wabunifu kutoka kila kona mbalimbali za dunia kwa lengo la kujadili maendeleo ya tasnia ya muziki barani afrika na dunia kwa ujumla na kutoa fursa za ushirikiano na ubadilishanaji wa maarifa.
Kwa jukwaa hilo, Frida Amani atatumbuiza pamoja na wasanii nyota kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Focalistic (Afrika kusini), Boukuru (Rwanda), Bokani (Afrika kusini) Njoki Karu ( kenya) na wengine wengi.
Ushiriki wa Frida Amani kwenye tamasha hili ni hatua kubwa kwa mziki wa Hiphop na Bongo Fleva na unatoa nafasi ya kipekee kuitangaza Tanzania kupitia muziki wa live performance, ubunifu na utamaduni wa kisasa unaobeba ujumbe ujumbe chanya kwa jamii