Nandy ameonesha kuwa anaufahamu ulimwengu wa utandawazi, ambapo kwa sasa muziki unakutana na teknolojia kwa kasi isiyozuilika.
Kupitia wimbo wake mpya “Sweet” akiwa na Jux, ameamua kusimama kidete, sio tu kama msanii, bali kama mbunifu na mtu makini kwenye promosheni.
Video ya “Sweet”, ambayo imetengenezwa kwa kutumia AI, sio jaribio la kisanaa bali ni tangazo la mapinduzi. Ndani yake kuna love story, lakini nyuma ya pazia kuna falsafa kubwa ya kimkakati, kutumia teknolojia kama lugha mpya ya hisia. Nandy anaonyesha kwamba muziki hautakiwi kusikika tu, unapaswa kuhisiwa, kuonwa na kuuishi.
Kwa siku moja tu, wimbo huu umevuka watamaji milioni 1 ndani ya siku moja, ishara tosha kwamba ubunifu hauhitaji kupigiwa debe kwa maneno bali unajieleza. Nandy ameamua kuunganisha sanaa na akili za kizazi kipya, na matokeo yake.
Huu ni uthibitisho kwamba “Sweet” sio tu wimbo, ni somo la kimkakati kwa wasanii wote wanaotaka kuelewa nguvu ya kusimulia hadithi, teknolojia na ushawishi.
Kwa Nandy, huu ni mwanzo wa sura mpya, ambapo muziki unakutana na akili ya ubunifu na dunia inasikiliza.