Baada ya ukimya wa mda mrefu, msanii wa Bongofleva, 20 percent ameibuka na kusema hajarogwa kama baadhi ya watu wanavyodai na amewataka mashabiki kuacha mambo ya uzushi.
20 percent ambaye aliwahi kuteka nyoyo za Mashabiki wengi kupitia nyimbo zenye jumbe fupi za kijamii, amesema ukimya wake umetokana na ubize wa majukumu mengine hivyo sasa amerudi rasmi kwenye anga la muziki na kuachia wimbo unaitwa ‘Ni Upendo’ pamoja na video yake.
Percent amesema “kwasasa nimeamua kurudi kwenye muziki nimeachia wimbo wangu unaoitwa ‘Ni Upendo’ na video yake pia, maana nimeona mashabiki wangu wamekuwa wakiniulizia sana kuhusu kama nimeacha muziki au vipi, na wapo ambao wanasema nimerogwa ndio maana nipo kimya ila ukweli sijarogwa na siamini Imani za kishirikina mimi, kukaa kwangu kimya ni majukumu ya hapa na pale yamenizidi”.