Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki zoezi la Medani wakati wa shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Pongwe Msungura, Msata Mkoani Pwani tarehe 23 Agosti, 2024.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake haitakiwi kuamrishwa, kupewa masharti, au kuelekezwa namna ya kuendesha majadiliano na wadau wa siasa.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Desemba 2, 2025, alipokutana nakuzungumzan na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), kuhusu hali ya kisiasa na matukio ya vurugu baada ya uchaguzi wa 2025.
Amesisitiza kuwa Tanzania ni taifa huru linalojiongoza kwa misingi ya mamlaka yake kamili na si kundi la watu linaloweza kushinikizwa.
Rais Samia amesema kumekuwapo taarifa za baadhi ya makundi ya kisiasa na watu wanaoendelea kutoa masharti kabla ya kukubali kukaa meza moja kufanya mazungumzo, ikiwamo masharti ya “mfanye hili”, “mwachie huyu”, au “tekelezeni kigezo hiki kabla ya kuzungumza.”
Amesema Serikali yake si ya kuamrishwa wala kupewa maelekezo nakwamba , mazungumzo yanayokusudiwa ni yale ya kuheshimiana na kutambua nafasi ya kila upande.