Watu watano wamekamatwa kwa tuhuma za kushiriki njama za kuficha Ukweli wa tuhuma za Afisa Tabibu msaidizi kumbaka mgonjwa wake Novemba 24 mwaka huu Hospitali ya Urambo mkoani Tabora.
Watano hao wanaingia katika sakata hilo wakijaribu kuficha ukweli wa tukio la Juma Selemani anayedaiwa kumbaka mgonjwa wake na hospitalini hapo na wana tuhuma mbalimbali zinazo ambatana na tukio hilo.
Watuhumiwa hao ni Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. David Manyama, na wengine wanne wanadaiwa kuficha ukweli na kutenda makosa mengine kinyume na maadili ya kazi na taratibu za utumishi wa umma.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul chacha akizungumza katika kikao maalumu ameeleza kuwa mtuhumiwa Juma Seleman amekuwa na destu ya kuwaingilia wanawake katika chumba cha upasuaji mara kadhaa toka mwaka 2018 jambo mabalo ni tabia endelevu licha ya kuonywa mara kadhaa.
Baadhi ya wahusika wanashikiliwa na Polisi na wengine wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, ili kuhakikisha haki inapatikana na uchunguzi unafanyika bila ushawishi au kuingiliwa.