Aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Luhanga Mpina, ameibuka na kutoa tuhuma dhidi ya Serikali, vyombo vya dola na taasisi za uchaguzi, akidai kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, mauaji na uonevu uliodaiwa kutokea wakati wa uchaguzi na maandamano yaliyofuatia.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mpina amesema matukio ya vurugu na vifo vya raia vinavyodaiwa kutokea siku ya uchaguzi “haviwezi kufumbiwa macho”
Katika hatua nyingine, Mpina ameishukuru jumuiya ya kimataifa, mashirika ya haki za binadamu na vyombo vya habari vya kimataifa kwa kulaani kile alichokiita ukiukwaji wa haki za binadamu, huku akizipongeza balozi 17 zilizotoa taarifa zao kuhusu matukio hayo.
Katika mapendekezo yake, Mpina ameitaka Serikali kuchukua hatua kadhaa ikiwamo, Kufuta uchaguzi ndani ya siku 90 na kurudia uchaguzi upya, Kuwajibisha viongozi wa juu akiwamo Rais, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais,Kuundwa kwa tume mpya huru ya uchaguzi,
Kuitishwa kwa kikao cha dharura cha EAC, SADC na AU,Kuvunjwa kwa tume ya uchunguzi iliyoanzishwa na Serikali kwa madai kwamba “haina uhalali wala imani ya wananchi.”