Staa wa Muziki wa Marekani TreySongz anaripotiwa kukamatwa na Polisi New York baada ya kudaiwa kumpiga mfanyakazi wa Club usoni, kufuatia mvutano ulioibuka walipoarifiwa kuwa Club hiyo ingefungwa saa 10 alfajiri (4:00 a.m.) tarehe 4 Desemba.
Waendesha mashtaka wa Manhattan wanasema tukio hilo lilisababisha mfanyakazi huyo kupata uvimbe na maumivu makali.
TreySongz (41) alifikishwa mahakamani na anakabiliwa na shtaka la shambulio, pamoja na kesi nyingine ya uharibifu wa mali isiyohusiana na tukio hilo. Anatarajiwa kurejea mahakamani Februari 2026.