Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV ametoa mwito wa kusitishwa mapigano kwenye mizozo yote duniani wakati wa sikukuu ya Krismasi kesho.
Akiwa kwenye makaazi yake ya mapumziko nje ya mji wa Roma, Baba Mtakatifu Leo amesema anarejea ombi lake kwa watu wote wenye nia njema kuifanya Krismasi kuwa siku ya amani, kwa kuonesha heshima kwa siku hiyo ya kuzaliwa Yesu Kristo.
Papa Leo pia amesikikitishwa na Urusi kukataa kuweka chini silaha katika vita vinavyoendeleanchini Ukrain hata wakati wa sherehe za sikukuu ya Krismasi.
Papa Leo wa XIV ametoa rai hiyo wakati ambao Wakristo kote duniani watasherehekea sikukuu ya Krismasi kesho kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu zaidi miaka 2000 iliyopita.
Sikukuu hii huambatana na shukrani, zawadi furaha ya kuwa pamoja kwa wanajamii kama ishara ya Ukombozi wa mwanadamu.