
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23, yaliyokuwa yafanyike mjini Doha yameahirishwa.
Pande zote mbili katika mgogoro wa Mashariki mwa Kongo, serikali na M23 zimethibitisha kwa shirika la habari la Reuters, kuahirishwa mkutano wao wa ana kwa ana mjini Doha.
Hata hivyo hakuna tarehe mpya iliyotolewa kwa mazungumzo mapya kufanyika.
Mapema mwezi huu wa Aprili, pande hizo mbili zilitangaza mkutano huo ambao ni wa kwanza tangu wapiganaji wa M23 walipoidhibiti miji miwili mikubwa nchini Kongo ya Bukavu na Goma.