
Idara ya udhibiti wa shule wilayani Nyang’whale mkoani Geita imesema itaendelea kusimamia sheria na kununi kuhakikisha kiwango cha utoaji wa elimu kinaendana na matakwa ya serikali
Mdhibiti mkuu ubora wa shule wilaya ya Nyang’whale Musa Hingila ameeleza hayo akiwa ofisini kwake kuhusu mikakati ya kuhakikisha elimu inatolewa katika ubora unaotakiwa
Amesema idara inasimamia vigezo vilivyowekwa vikiwemo, ubora wa mitaala, ufundishaji na uongozi sambamba na maadili yanayofundishwa kwa wanafunzi
Aidha Hingila amesema pia idara hiyo imekuwa ikifuatilia uanzishwaji wa shule za watu binafsi ili waendane na mitaala inayotolewa na serikali pamoja na mazingira rafiki ya kujifunzia